Hot!

Kauli ya Wadau Kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Mifugo Tanzania



Wadau wa sekta ya mifugo wametoa kauli kuhusu maendeleo ya sekta ya mifugo tanzania. Kwa kuzingatia fursa zilizopo katika sekta ya mifugo na ukweli kuwa Tanzania inashika nafasi ya tatu (baada ya Ethiopia na Sudani) kwa idadi ya mifugo; wadau wanaona kuwa bado sekta ya mifugo haifanyi vizuri katika kuchangia pato la taifa kama inavyostahili, na ipo haja ya kufanya mabadiliko na uhamasishaji katika sekta hii
Hivyo basi muunganiko wa asasi za kiraia, wafugaji, watafiti, watu binafsi, vyama vya wakulima na wadau wengine chini ya Jukwaa Huru la Wadau wa Kilimo na Asasi Zisizo za Kiserekali (Agriculture Non State Actors Forum (ANSAF)); kwa pamoja wametia saini kauli yenye mapendekezo yafuatayo:
·         Kutambua kwa mapana mchango mkubwa wa mifugo kwa uchumi wa taifa na hivyo kutafsiriwa katika ongezeko la uwekezaji na sekta binafsi kuisaidia sekta hii
·         Kuongeza ushiriki wa wadau wasio wa kiserekali katika kutambua na kuunda sera za mifugo rafiki kwa wakulima wadogo wadogo na wafugaji wa asili nchini
·         Ushiriki wa wanawake na vijana katika mnyororo wa mifugo
·        Kuwakilisha uwajibikaji wa wawekezaji wa sekta binafsi katika kutekeleza ushirikishwaji wa wakulima wadogowadogo na wafugaji wa asili kuhusu fursa za maendeleo katika sekta ya mifugo
Kwa kupata nakala halisi ya tamko bofya hapa:

0 comments:

Post a Comment